Aug 20, 2025
NOVENA KWA MT.RITA WA KASHIA
NOVENA SIKU YA KWANZA
Kwa jina la Baba, na la Mwana na la Roho Mtakatifu. Amina.
Ee Mtakatifu Rita mfanya miujiza, uniangalie kwa macho yako yenye huruma, mimi ninaye teseka
na kutoa machozi. Uone moyo wangu unaotoka damu umezungukwa na miiba. Yaonr macho yangu, ee
Mtakatifu Rita, kuwa hayatoki machozi tena kwani machozi mengi yamenitoka!
Nimechoka na kukata tamaa. Nimechoka pia kusali. Je, nikate tamaa katika misukosuko hii ya
maisha yangu? Uje! Ee Mtakatifu Rita, njoo hima unisaidie. Je, wakristo hawakuiti Mtakatifu wa mambo
yaliyoshindikana na mwombezi wa waliokata tamaa? Basi dhihirisha ukuu wa jina hilo, kwa kunijalia toka
kwa Mungu yote ninayokuomba (hapa omba hitaji lako unalotaka kumwomba Mungu kupitia
Mtakatifu Rita).
Kila mtu anasifia utakatifu wako. Kila mtu anasimulia maajabu na miujiza Mungu anayotenda kwa
njia yako. Je, mimi tu nitakataliwa na kukatishwa tamaa kwa vile hujanisikia? Hapana. Uniombee kwa
Bwana Yesu ili anionee huruma na kunisaidia katika masumbuko na mahangaiko yangu. Kwa maombezi
yako, Ee Mtakatifu Rita, niweze kupokea kile ambacho moyo wangu unatamani sana.
Baba yetu ×3 Salamu Maria ×3 na Atukuzwe Baba ×3
Kwa njia ya Mtakatifu Rita: - homa, madonda na tauni, viini vya maradhi mbalimbali, mapepo na
ghadhabu vitoweke. Unawasaidia vipofu, viziwi, bubu na viwete: watoto wanaomba sana na wafu
wanarudishiwa uhai.
Kwa maombezi yako: - radi, tetemeko la ardhi na moto havina nguvu. Kwa utakatifu wako mitego
yote, hatari kubwa na vitisho vyote hutoweka. Unawasaidia vipofu, viziwi, bubu na viwete: watoto
wanaomba sana na wafu wanarudishiwa uhai.
Hispania wanakutangaza kuwa Mtakatifu wa mambo yaliyoshindikana. Watu wengi wanaimba sifa
zako. Kashia hutukusa jina lako. Unawasaidia vipofu, viziwi, bubu na viwete: watoto wanaomba sana
na wafu wanarudishiwa uhai.
Kwa Mungu Mtakatifu na kwa Mwanae ziwe sifa, utukufu na heshima, sifa kwa karne zote za pendo
la milele. Unawasaidia vipofu, viziwi, bubu na viwete: watoto wanaomba sana na wafu
wanarudishiwa uhai.
Kiongozi: Umemtia alama Ee Bwana, mtumishi wako Rita.
Wote: Kwa mhuri wa upendo na mateso.
TUOMBE
Ee Mungu, uliyekubali kumtawadha Mtakatifu Rita kwa neema, hata akakubali kuwapenda adui zake hadi
akapata rohoni mwake na katika paji la uso alama za upendo na mateso. Tunakuomba kupitia maombezi
yake, neema za za kusamehe adui zetu na kutafakari maumivu ya mateso yako, ili tupate tuzo ulilotuahidia
kwa wapole na wanaoteseka. Unayeishi na kutawala, daima na milele. Amina.
Litania Kwa Mtakatifu Rita wa Kashia....... (Bonyeza hapa)
© Mkatoliki Kiganjani. Haki Zote Zimehifadhiwa.